Posts

Aua na yeye kujiua

Image
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi amesema kuwa mtu huyo ametambulika kwa jina la John Ntemi (23) mkazi wa Kijiji cha Mahaha ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe Casta Edward. Aidha, Kamanda Msangi amesema inadaiwa wawili hao walikuwa wanaishi peke yao na kabla ya tukio hilo kutokea wanandoa hao walikuwa wakiishi kwa amani na upendo bila ya mgogoro wa aina yeyote kati yao, lakini ilipofikia Machi 26, 2018 majira ya saa 6:00 mchana mwenye nyumba waliyopanga alipita karibu na maeneo ya nyumba yao ndipo alipoona damu chini ya mlango, na kuweza kutoa taarifa kwa majirani pamoja na Jeshi la Polisi. Pamoja na hayo, Kamanda Msangi amesema polisi walipofika katika eneo la tukio waliweza kukuta mwili wa mwanamke ukiwa mlangoni ndani ya nyumba eneo la tukio likionesha miburuzo ya damu toka chumbani hadi mlangoni huku mlango ukiwa umefungwa kwa kufuli. Uchunguzi wa awali unaonesha mauji hayo yalitekelezwa usiku wa Machi 2...

Samata afunguka haya kuhu Taifa Stars

Image
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumanne ya March 27 2018 ilicheza game yake ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Congo DRC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo ulimalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli yakifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 74 na Shiza Kichuya dakika ya 85. Baada ya game AyoTV iliongea na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta aelezee game hiyo baada ya ushindi huo, ikiwa ni siku tano zimepita toka Taifa Stars wapoteza dhidi ya Algeria kwa magoli 4-1, Samatta ameuelezea mchezo huo na kueleza kuwa Tanzania inahitaji wachezaji wengi professional ili izidi kufanya vizuri. “Game mbili tulizocheza dhidi ya Algeria na Congo ni game ngumu lakini kama hivyo unavyopata matokeo unakuwa umejisogeza kiasi fulani na hata ukikosa matokeo vile vile inakujengea kujiamini” Tanzania vipi inahitaji kocha wa kigeni kwa sasa? “No comment hilo siwezi kulizungumzia”

waziri mwigulu nchemba azungumza haya kwa viongozi waserikali

Image
Amesema ongezeko la wahamiaji haramu limepelekea serikali kuweka mitego ya kisasa kuwabaini wahusika wa vitendo hivyo. Waziri Nchemba amesema njia hizo ambazo zimepelekea ongezeko la kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao ni pamoja na kuweka ushiriki wa nchi jirani katika mitego hiyo ambazo ndio njia za wahamiaji hao kupita na kuwachukulia hatua kali za kisheria watendaji wa serikali walioshiriki kutekeleza zoezi hilo ambalo linakiuka sheria za nchi. Kuhusu vifaa vinavyotumika kuwasafirishia wahamiaji hao haramu Nchemba amesema tayari wametaifisha mali za wahusika hao na kuzimilikisha kwa serikali ili kutoa adhabu kwa wamiliki hao kuogopa kuwapa magari yao watu wasiowaamini na katika kutelekeza hilo serikali haitakua na huruma nao.

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

Image
Mabingwa wa Ufaransa Monaco ndiyo klabu ya karibuni zaidi kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ubelgiji unamalizika mwisho wa msimu na anatarajiwa kuondoka Old Trafford. (Mail) Dani Ceballos ambaye amekuwa akitafutwa na Liverpool ameambia anaweza kutoka Real Madrid mwisho wa msimu. Kiungo huyo wa kati Mhispania wa miaka 21 amekuwa pia anatafutwa na AC Milan na Juventus. (Mundo Deportivo kupitia Talksport) Kipa Mbelgiji Simon Mignolet, 30, amesema atasalia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza Liverpool na hatalazimishwa kuondoka klabu hiyo. (Sun) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema anataka sana kiungo wa kati Jack Wilshere asalie katika klabu hiyoo. Mchezaji huyo wa England wa miaka 26 amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba baada yake kuombwa akubali kupunguziwa mshahara. (Star) Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel angependa zaidi kwenda Bayern ...

Kifaru mzee aliyefariki kufanyiwa sherehe yakumuenzi

Image
Wiki iliyopita Kifaru Sudan ambaye ndiye alikuwa kifaru mzee zaidi wa kiume aliyebaki duniani ambaye alikuwa anapatikana katika Hifadhi ya Ol Pejeta nchini Kenya aliripotiwa kufa. Kutokana na kifaru huyo kuwa wa pekee duniani, inaandaliwa sherehe maalumu kwa ajili ya kumbukumbu yake na kusherekea kipindi cha maisha yake, ambayo itafanyika March 31, 2018. Kwenye barua maalumu ya mwaliko kwa vyombo vya habari kutoka kwa Uongozi wa Hifadhi hiyo na Wizara ya Utalii imeeleza kuwa sherehe hiyo itahudhuriwa pia na Katibu wa Wizara wa Utalii Najib Balala. Sherehe hiyo itafanyika eneo la ‘Uwanja wa Kumbukumbu ya Kifar

Messi amemtumia salamu hizo Neymar,

Image
Messi amemtumia salamu hizo Neymar, huku akimwambia ni vyema akajiunga na Manchester City ya England, kwa kuwa anatambua huko atakua na maisha mazuri zaidi kuliko Hispania, tena akiwa na timu pinzani na aliyowahi kuitumikia nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida Don Balon ambalo limeandika taarifa za mshambuliaji huyo kumshauri Naymar, zinaeleza kwamba harakati hizo za Messi ni kutaka kumuunganisha mchezaji huyo wa kibrazil na Pep Guardiola ambaye kwa sasa ndio mkuu wa benchi la ufundi huko Etihad Stadium. Telstar 18 wamchukiza David de Gea Messi ameliambia jarida hilo kuwa, anaamini Neymar atakua mwenye furaha zaidi kama atakua chini ya meneja Guardiola, kutokana na kumtambua vilivyo, huku akiwakandia Real Madrid kwa kusema hawatoweza kumtunzia kipaji chake ipasavyo. Joe Gomez kuikosa Italia Kocha Taifa Stars atamba kuibuka na ushindi dhidi ya DR Congo, kesho. Neymar, mwenye umri wa miaka 26, alisajiliwa na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu uliopit...

Gambo aomba ushirikiano na viongozi wa CHADEMA bila kujali itikadi zao

Image
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka viongozi wa CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali. Gambo ameyasema hayo baada ya viongozi hao wa CHADEMA ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lililokuwa likisimamiwa na serikali. “Nipende kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali, mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli,”amesema Gam...