TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

Mabingwa wa Ufaransa Monaco ndiyo klabu ya karibuni zaidi kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ubelgiji unamalizika mwisho wa msimu na anatarajiwa kuondoka Old Trafford. (Mail)

Dani Ceballos ambaye amekuwa akitafutwa na Liverpool ameambia anaweza kutoka Real Madrid mwisho wa msimu. Kiungo huyo wa kati Mhispania wa miaka 21 amekuwa pia anatafutwa na AC Milan na Juventus. (Mundo Deportivo kupitia Talksport)

Kipa Mbelgiji Simon Mignolet, 30, amesema atasalia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza Liverpool na hatalazimishwa kuondoka klabu hiyo. (Sun)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema anataka sana kiungo wa kati Jack Wilshere asalie katika klabu hiyoo. Mchezaji huyo wa England wa miaka 26 amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba baada yake kuombwa akubali kupunguziwa mshahara. (Star)

Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel angependa zaidi kwenda Bayern Munich kurejelea kazi ya ukufunzi na si kwenda Arsenal, kama zilivyokuwa zimedokeza tetesi kwamba atakwenda kumrithi Wenger. (Sky Sports)Thomas Tuchel

Kiungo wa kati wa Liverpool kutoka Ujerumani Emre Can, 24, amelazimika kuandika kwenye Instagram ujumbe wa kupuuzilia mbali uvumi kwamba anataka kuondoka Anfield.

Meneja wa Manchester United Mourinho ameandaa orodha ya wachezaji sita ambao anaamini wanaweza kujaza nafasi ya Michael Carrick anayeelekea kustaafu. Orodha hiyo inashirikisha nyota wa Bayern Munich kutoka Chile Arturo Vidal, 30, na Mwitaliano anayechezea Paris St-Germain Marco Verratti, 25. (Manchester Evening News)

United wataimarisha juhudi zao za kutaka kumnunua beki wa Celtic ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £25m Kieran Tierney mwisho wa msimu. Mourinho anataka sana beki huyo wa miaka 20 mzaliwa wa Manx, Scotland ajiunge na klabu hiyo na anatarajiwa kuwasilisha ofa karibuni. (Mirror)

Comments

Popular posts from this blog

mengine yaibuka sakata la wambura

London fire: 58 missing, presumed dead - police