Posts

Showing posts with the label Michezo

Samata afunguka haya kuhu Taifa Stars

Image
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jumanne ya March 27 2018 ilicheza game yake ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya Congo DRC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo ulimalizika kwa Taifa Stars kupata ushindi wa magoli 2-0, magoli yakifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 74 na Shiza Kichuya dakika ya 85. Baada ya game AyoTV iliongea na nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta aelezee game hiyo baada ya ushindi huo, ikiwa ni siku tano zimepita toka Taifa Stars wapoteza dhidi ya Algeria kwa magoli 4-1, Samatta ameuelezea mchezo huo na kueleza kuwa Tanzania inahitaji wachezaji wengi professional ili izidi kufanya vizuri. “Game mbili tulizocheza dhidi ya Algeria na Congo ni game ngumu lakini kama hivyo unavyopata matokeo unakuwa umejisogeza kiasi fulani na hata ukikosa matokeo vile vile inakujengea kujiamini” Tanzania vipi inahitaji kocha wa kigeni kwa sasa? “No comment hilo siwezi kulizungumzia”

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA

Image
Mabingwa wa Ufaransa Monaco ndiyo klabu ya karibuni zaidi kuonesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 kutoka Ubelgiji unamalizika mwisho wa msimu na anatarajiwa kuondoka Old Trafford. (Mail) Dani Ceballos ambaye amekuwa akitafutwa na Liverpool ameambia anaweza kutoka Real Madrid mwisho wa msimu. Kiungo huyo wa kati Mhispania wa miaka 21 amekuwa pia anatafutwa na AC Milan na Juventus. (Mundo Deportivo kupitia Talksport) Kipa Mbelgiji Simon Mignolet, 30, amesema atasalia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha kwanza Liverpool na hatalazimishwa kuondoka klabu hiyo. (Sun) Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema anataka sana kiungo wa kati Jack Wilshere asalie katika klabu hiyoo. Mchezaji huyo wa England wa miaka 26 amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba baada yake kuombwa akubali kupunguziwa mshahara. (Star) Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel angependa zaidi kwenda Bayern ...

Messi amemtumia salamu hizo Neymar,

Image
Messi amemtumia salamu hizo Neymar, huku akimwambia ni vyema akajiunga na Manchester City ya England, kwa kuwa anatambua huko atakua na maisha mazuri zaidi kuliko Hispania, tena akiwa na timu pinzani na aliyowahi kuitumikia nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida Don Balon ambalo limeandika taarifa za mshambuliaji huyo kumshauri Naymar, zinaeleza kwamba harakati hizo za Messi ni kutaka kumuunganisha mchezaji huyo wa kibrazil na Pep Guardiola ambaye kwa sasa ndio mkuu wa benchi la ufundi huko Etihad Stadium. Telstar 18 wamchukiza David de Gea Messi ameliambia jarida hilo kuwa, anaamini Neymar atakua mwenye furaha zaidi kama atakua chini ya meneja Guardiola, kutokana na kumtambua vilivyo, huku akiwakandia Real Madrid kwa kusema hawatoweza kumtunzia kipaji chake ipasavyo. Joe Gomez kuikosa Italia Kocha Taifa Stars atamba kuibuka na ushindi dhidi ya DR Congo, kesho. Neymar, mwenye umri wa miaka 26, alisajiliwa na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu uliopit...

Njombe mji fc watoa taarifa game yao na simba

Image
Uongozi wa Njombe Mji FC umesema haujapokea taarifa yeyote kuhusu mabadiliko ya terehe mchezo dhidi ya Simba kupangwa kucheza Aprili 3 2018. Kwa mujibu wa Msemaji wa Njombe Mji, Hassan Macho, amesema kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari, mpaka sasa hazina uthibitisho wowote. "Kanuni ya ligi kuu inatamka kwamba taarifa za mabadiliko ya mchezo zitatolewa kwa klabu siku 14 kabla ya mchezo husika. Timu ya Njombe mji haijapokea taarifa kuhusu mchezo huo kuchezwa tarehe 3.4.2018" ameeleza. "Hii itakuwa njia ya kutuondoa kwenye ligi, haiwezekani tukacheze Shinyanga siku mbili halafu turudi Njombe kisha turudi tena Shinyanga siku mbili baadae. Kanuni inataka tupate taarifa siku kumi na nne leo hata tukipewa kesho basi siku hizo hazikidhi kwa mujibu wa kanuni" amesema Macho. Timu hiyo kwa sasa inajiandaa na safari kuelekea Shinyanga kwa michezo miwili dhidi ya Stand United. Ratiba iliyopo mpaka sasa iko hivi Stand United vs N...